8 Uniondolee ubatili na uongo;Usinipe umaskini wala utajiri;Unilishe chakula kilicho kadiri yangu.
9 Nisije nikashiba nikakukana,Nikasema, BWANA ni nani?Wala nisiwe maskini sana nikaiba,Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.
10 Usimchongee mtumwa kwa bwana wake;Asije akakulaani, ukaonekana una hatia.
11 Kuna kizazi cha watu wamlaanio baba yao;Wala hawambariki mama yao.
12 Kuna kizazi cha watu walio safi machoni pao wenyewe;Ambao hawakuoshwa uchafu wao.
13 Kuna kizazi cha watu ambao macho yao yameinuka kama nini!Na kope zao zimeinuka sana.
14 Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga;Na vigego vyao ni kama visu.Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu.