13 Hutafuta sufu na kitani;Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.
14 Afanana na merikebu za biashara;Huleta chakula chake kutoka mbali.
15 Tena huamka, kabla haujaisha usiku;Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula;Na wajakazi wake sehemu zao.
16 Huangalia shamba, akalinunua;Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
17 Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi;Hutia mikono yake nguvu.
18 Huona kama bidhaa yake ina faida;Taa yake haizimiki usiku.
19 Hutia mikono yake katika kusokota;Na mikono yake huishika pia.