20 Huwakunjulia maskini mikono yake;Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
21 Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake;Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
22 Hujifanyia mazulia ya urembo;Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
23 Mume wake hujulikana malangoni;Aketipo pamoja na wazee wa nchi.
24 Hufanya nguo za kitani na kuziuza;Huwapa wafanya biashara mishipi.
25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake;Anaucheka wakati ujao.
26 Hufumbua kinywa chake kwa hekima,Na sheria ya wema i katika ulimi wake.