25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake;Anaucheka wakati ujao.
26 Hufumbua kinywa chake kwa hekima,Na sheria ya wema i katika ulimi wake.
27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake;Wala hali chakula cha uvivu.
28 Wanawe huondoka na kumwita heri;Mumewe naye humsifu, na kusema,
29 Binti za watu wengi wamefanya mema,Lakini wewe umewapita wote.
30 Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili;Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.
31 Mpe mapato ya mikono yake,Na matendo yake yamsifu malangoni.