19 Njia ya waovu ni kama giza;Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho.
20 Mwanangu, sikiliza maneno yangu;Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu.
21 Zisiondoke machoni pako;Uzihifadhi ndani ya moyo wako.
22 Maana ni uhai kwa wale wazipatao,Na afya ya mwili wao wote.
23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
24 Kinywa cha ukaidi ukitenge nawe,Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.
25 Macho yako yatazame mbele,Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa.