2 Kwa kuwa nawapa mafundisho mazuri;Msiiache sheria yangu.
3 Maana nalikuwa mwana kwa baba yangu,Mpole, mpenzi wa pekee wa mama yangu.
4 Naye akanifundisha, akaniambia,Moyo wako uyahifadhi maneno yangu;Shika amri zangu ukaishi.
5 Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau;Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu.
6 Usimwache, naye atakuhifadhi;Umpende, naye atakulinda.
7 Bora hekima, basi jipatie hekima;Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
8 Umtukuze, naye atakukuza;Atakupatia heshima, ukimkumbatia.