20 Mwanangu, sikiliza maneno yangu;Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu.
21 Zisiondoke machoni pako;Uzihifadhi ndani ya moyo wako.
22 Maana ni uhai kwa wale wazipatao,Na afya ya mwili wao wote.
23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
24 Kinywa cha ukaidi ukitenge nawe,Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.
25 Macho yako yatazame mbele,Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa.
26 Ulisawazishe pito la mguu wako,Na njia zako zote zithibitike;