4 Naye akanifundisha, akaniambia,Moyo wako uyahifadhi maneno yangu;Shika amri zangu ukaishi.
5 Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau;Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu.
6 Usimwache, naye atakuhifadhi;Umpende, naye atakulinda.
7 Bora hekima, basi jipatie hekima;Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
8 Umtukuze, naye atakukuza;Atakupatia heshima, ukimkumbatia.
9 Atakupa neema kuwa kilemba kichwani;Na kukukirimia taji ya uzuri.
10 Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu;Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi.