5 Miguu yake inatelemkia mauti;Hatua zake zinashikamana na kuzimu;
6 Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima;Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari.
7 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa,Wala msiache maneno ya kinywa changu.
8 Itenge njia yako mbali naye,Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake.
9 Usije ukawapa wengine heshima yako,Na wakorofi miaka yako;
10 Wageni wasije wakashiba nguvu zako;Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni;
11 Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho,Nyama yako na mwili wako utakapoangamia;