4 Usiache macho yako kupata usingizi,Wala kope za macho yako kusinzia.
5 Ujiponye kama paa na mkono wa mwindaji,Na kama ndege katika mkono wa mtega mitego.
6 Ewe mvivu, mwendee chungu,Zitafakari njia zake ukapate hekima.
7 Kwa maana yeye hana akida,Wala msimamizi, wala mkuu,
8 Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua;Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.
9 Ewe mvivu, utalala hata lini?Utaondoka lini katika usingizi wako?
10 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,Bado kukunja mikono upate usingizi!