19 Maana mume wangu hayumo nyumbani,Amekwenda safari ya mbali;
20 Amechukua mfuko wa fedha mkononi;Atarudi wakati wa mwezi mpevu.
21 Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi,Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda.
22 Huyo akafuatana naye mara hiyo,Kama vile ng’ombe aendavyo machinjoni;Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu;
23 Hata mshale umchome maini;Kama ndege aendaye haraka mtegoni;Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.
24 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa,Mkayaangalie maneno ya kinywa changu.
25 Moyo wako usizielekee njia zake,Wala usipotee katika mapito yake.