3 Zifunge katika vidole vyako;Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
4 Mwambie hekima, Wewe ndiwe umbu langu;Mwite ufahamu jamaa yako mwanamke.
5 Wapate kukulinda na malaya,Na mgeni akubembelezaye kwa maneno yake.
6 Maana katika dirisha la nyumba yanguNalichungulia katika shubaka yake;
7 Nikaona katikati ya wajinga,Nikamtambua miongoni mwa vijana,Kijana mmoja asiyekuwa na akili,
8 Akipita njiani karibu na pembe yake,Akiishika njia iendayo nyumbani kwake,
9 Wakati wa magharibi, wakati wa jioni,Usiku wa manane, gizani.