2 Juu ya mahali palipoinuka karibu na njia,Penye njia panda, ndipo asimamapo.
3 Karibu na malango, mahali pa kuingia mjini,Mahali pa kuyaingilia malango anapiga kelele.
4 Enyi watu, nawaita ninyi;Na sauti yangu ni kwa wanadamu.
5 Enyi wajinga, fahamuni werevu,Nanyi wapumbavu, mpate moyo wa kufahamu.
6 Sikieni, maana nitasema yaliyo mazuri,Na kufumbua midomo yangu kutakuwa maadili.
7 Maana kinywa changu kitasema kweli,Na uovu ni chukizo kwa midomo yangu.
8 Maneno yote ya kinywa changu yana haki;Hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi.