23 Nalitukuka tokea milele, tangu awali,Kabla haijawako dunia.
24 Wakati visipokuwako vilindi nalizaliwa,Wakati zisipokuwako chemchemi zilizojaa maji.
25 Kabla milima haijawekwa imara,Kabla ya vilima nalizaliwa.
26 Alipokuwa hajaiumba dunia, wala makondeWala chanzo cha mavumbi ya dunia;
27 Alipozithibitisha mbingu nalikuwako;Alipopiga duara katika uso wa bahari;
28 Alipofanya imara mawingu yaliyo juu;Chemchemi za bahari zilipopata nguvu;
29 Alipoipa bahari mpaka wake,Kwamba maji yake yasiasi amri yake;Alipoiagiza misingi ya nchi;