26 Alipokuwa hajaiumba dunia, wala makondeWala chanzo cha mavumbi ya dunia;
27 Alipozithibitisha mbingu nalikuwako;Alipopiga duara katika uso wa bahari;
28 Alipofanya imara mawingu yaliyo juu;Chemchemi za bahari zilipopata nguvu;
29 Alipoipa bahari mpaka wake,Kwamba maji yake yasiasi amri yake;Alipoiagiza misingi ya nchi;
30 Ndipo nilipokuwa pamoja naye, kama stadi wa kazi;Nikawa furaha yake kila siku;Nikifurahi daima mbele zake;
31 Nikiifurahia dunia inayokaliwa na watu;Na furaha yangu ilikuwa pamoja na wanadamu.
32 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa;Maana heri hao wazishikao amri zangu.