5 Enyi wajinga, fahamuni werevu,Nanyi wapumbavu, mpate moyo wa kufahamu.
6 Sikieni, maana nitasema yaliyo mazuri,Na kufumbua midomo yangu kutakuwa maadili.
7 Maana kinywa changu kitasema kweli,Na uovu ni chukizo kwa midomo yangu.
8 Maneno yote ya kinywa changu yana haki;Hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi.
9 Yote humwelea yule afahamuye,Yote huelekea mbele yao waliopata maarifa.
10 Pokea mafundisho yangu, wala si fedha,Na maarifa kuliko dhahabu safi.
11 Maana hekima ni bora kuliko marijani;Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo.