9 Yote humwelea yule afahamuye,Yote huelekea mbele yao waliopata maarifa.
10 Pokea mafundisho yangu, wala si fedha,Na maarifa kuliko dhahabu safi.
11 Maana hekima ni bora kuliko marijani;Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo.
12 Mimi, hekima, nimefanya werevu kuwa kao langu;Natafuta maarifa na busara.
13 Kumcha BWANA ni kuchukia uovu;Kiburi na majivuno, na njia mbovu,Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.
14 Shauri ni langu, na maarifa yaliyo sahihi;Mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu.
15 Kwa msaada wangu wafalme humiliki,Na wakuu wanahukumu haki.