4 Kila aliye mjinga na aingie humu.Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili,
5 Njoo ule mkate wangu,Ukanywe divai niliyoichanganya.
6 Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi,Mkaende katika njia ya ufahamu.
7 Amkemeaye mwenye dharau hujipatia fedheha;Amkaripiaye mtu mbaya hujipatia aibu.
8 Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia;Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda.
9 Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima;Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu;
10 Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima;Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.