3 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Damasko wametenda dhambi tena na tena;kwa hiyo, sitaacha kuwaadhibu;waliwatendea watu wa Gileadi ukatili mbaya.
4 Basi, nitaishushia moto ikulu ya mfalme Hazaeli,nao utaziteketeza kabisa ngome za mfalme Ben-hadadi.
5 Nitayavunjavunja malango ya mji wa Damasko,na kuwang'oa wakazi wa bonde la Aweni,pamoja na mtawala wa Beth-edeni.Watu wa Aramu watapelekwa uhamishoni Kiri.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
6 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Gaza wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Walichukua mateka watu kabila zima,wakawauza wawe watumwa kwa Waedomu.
7 Basi, nitazishushia moto kuta za mji wa Gaza,nao utaziteketeza kabisa ngome zake.
8 Nitawang'oa wakazi wa mji wa Ashdodi,pamoja na mtawala wa Ashkeloni.Nitanyosha mkono dhidi ya Ekroni,nao Wafilisti wote waliosalia wataangamia.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
9 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Tiro wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Walichukua mateka kabila zima hadi Edomu,wakaukiuka mkataba wa urafiki waliokuwa wamefanya.