4 Kwa hiyo, toa unabii dhidi yao! Tabiri ewe mtu!”
5 Kisha roho ya Mwenyezi-Mungu ikanijia, naye akaniambia, “Waambie watu, Mwenyezi-Mungu asema hivi: Naam, hiki ndicho mnachofikiri enyi Waisraeli. Najua mambo mnayofikiria moyoni mwenu.
6 Nyinyi mmewaua watu wengi mjini humu, na kujaza barabara zake na watu waliouawa.
7 “Lakini, mimi, Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Naam, mji huu ni chungu cha kupikia, na wale waliouawa ndio nyama. Nyinyi lazima mtaondolewa mjini.
8 Nyinyi mmeogopa upanga? Basi, mimi nitaleta upanga dhidi yenu!
9 Nitawatoa ndani ya mji na kuwatia mikononi mwa watu wa mataifa mengine, nami nitawahukumu.
10 Mtauawa kwa upanga, nami nitawahukumu mpakani mwa Israeli. Hapo ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.