1 Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:
2 “Wewe mtu! Tega kitendawili, uwaambie fumbo Waisraeli.
3 Waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Kulikuwa na tai mmoja mkubwa sanaaliyekuwa na mabawa makubwa,yenye manyoya marefu mengiyenye rangi za kila aina.Tai huyo aliruka mpaka mlimani Lebanoni,akatua juu ya kilele cha mwerezi;
4 akakwanyua tawi lake la juu zaidi,akalipeleka katika nchi ya wafanyabiashara,akaliweka katika mji wao mmoja.
5 Kisha akachukua mmea mchanga nchini Israeli,akaupanda katika ardhi yenye rutubaambako kulikuwa na maji mengi.
6 Mmea ukakua ukawa mzabibuwa aina ya mti utambaao;matawi yake yakamwelekea,na mizizi yake ikatanda chini yake.Mzabibu ukachipua matawi na majani mengi.
7 Lakini kulikuwa na tai mwingine mkubwa;alikuwa na mabawa makubwa ya manyoya mengi.Basi, ule mzabibu ukamtandia mizizi yake,ukamwelekezea matawi yake,ili aumwagilie maji.