2 “Wewe mtu! Andika tarehe ya siku ya leo, maana hii ni siku ambapo mfalme wa Babuloni anaanza kuuzingira mji wa Yerusalemu.
3 Wape mfano hao watu wangu waasi na kuwaambia kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema:Kiweke chungu juu ya meko,ukakijaze maji pia.
4 Tia humo vipande vya nyama,vipande vizuri vya mapaja na mabega.Kijaze pia mifupa mizuri.
5 Tumia nyama nzuri ya kondoo,panga kuni chini ya chungu,chemsha vipande vya nyama na mifupa,vyote uvichemshe vizuri.
6 “Basi, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Ole wake mji wa mauaji! Mji huo ni kama chungu chenye kutu, ambacho kutu yake haiwezi kutoka! Vipande vya nyama ndani yake hutolewa kimojakimoja bila kuchaguliwa.
7 Mauaji yamo humo mjini; damu yenyewe haikumwagwa udongoni ifunikwe na vumbi, ila ilimwagwa mwambani.
8 Damu hiyo nimeiacha huko mwambani ili isifunikwe, nipate kuamsha ghadhabu yangu na kulipiza kisasi.