23 Wakazi wa miji ya Harani, Kane na Edeni na wachuuzi wa Ashuru na Kilmadi walifanya biashara nawe.
24 Hao walifanya nawe biashara ya mavazi ya fahari, nguo za buluu zilizotariziwa, mazulia ya rangi angavu vifundo na kamba zilizosokotwa imara.
25 Merikebu za Tarshishi ndizo zilikusafirishia bidhaa zako.Basi kama meli katikati ya bahariwewe ulikuwa umejaa shehena.
26 Wapiga makasia wako walikupeleka mbali baharini.Upepo wa mashariki umekuvunjavunjaukiwa mbali katikati ya bahari.
27 Utajiri wako wa bidhaa na mali,wanamaji wako wote chomboni,mafundi wako wa meli na wachuuzi wako,askari wako wote walioko kwako,pamoja na wasafiri walioko kwako,wote wataangamia baharini,siku ile ya kuangamizwa kwako.
28 Mlio wa mabaharia wako utakaposikika,nchi za pwani zitatetemeka.
29 Hapo wapiga makasia wotewataziacha meli zao.Wanamaji na manahodha watakaa pwani.