5 Wanajeshi kutoka Persia, Kushi na Puti wako pamoja nao; wote wana ngao na kofia za chuma.
6 Pia vikosi kutoka Gomeri, Beth-togarma, upande wa kaskazini kabisa, na majeshi yao yote pamoja na majeshi kutoka mataifa mengine, yako pamoja nawe.
7 Jitayarishe, ukae wewe mwenyewe na jeshi lako lote pamoja na wengine wote ulio nao, ukawalinde.
8 “Baada ya siku nyingi utaitwa kuishambulia nchi ambayo watu wengi waliletwa kutoka mataifa mengi na sasa wanaishi bila vitisho vya vita. Utaishambulia milima ya Israeli ambayo hapo awali ilikuwa jangwa na mahame kwa muda mrefu, lakini sasa watu wote huko wanaishi kwa usalama.
9 Utakwenda kasi kama tufani na kuifunika nchi kama wingu, wewe mwenyewe na jeshi lako lote na mataifa mengi yaliyo pamoja nawe.
10 “Wewe Gogu! Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Siku ile itakapofika utaanza kuwaza moyoni mwako na kupanga mipango miovu na kusema:
11 ‘Nitakwenda kuishambulia nchi isiyo na kuta, nchi ambako wananchi wake wanaishi kwa amani. Wote wanakaa katika miji isiyo na kuta; hawana makomeo wala malango.’