14 Makuhani ambao watakuwa wamehudumu katika patakatifu, wanapotaka kwenda kwenye ua wa nje, ni lazima wayaache humo mavazi waliyovaa walipokuwa wanahudumu mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa sababu mavazi hayo ni matakatifu. Ni lazima wavae mavazi mengine kabla ya kutoka nje ambako watu wanakusanyika.”
15 Baada ya yule mtu kulipima eneo la ndani la nyumba ya Mwenyezi-Mungu, alinitoa nje kupitia lango la mashariki na kulipima eneo la nje.
16 Aliuchukua ule ufito wake wa kupimia na kuupima upande wa mashariki, nao ulikuwa mita 250.
17 Akaupima upande wa kaskazini kwa kutumia ufito wake, nao ulikuwa mita 250.
18 Kisha akaupima upande wa kusini kwa kutumia ufito wake, nao ulikuwa mita 250.
19 Kisha akageuka na kupima upande wa magharibi kwa kutumia ufito wake, nao ulikuwa mita 250.
20 Hivyo akawa amepima pande zote, nazo zilikuwa mita 250 kila upande. Ukuta huo ulitenganisha kati ya eneo takatifu na lile la kawaida.