6 Vile vyumba vya juu kabisa vilijengwa kwenye miinuko na havikusaidiwa na nguzo kama majengo mengine kwenye ua wa nje.
7 Kulikuwa na ukuta mkabala na vyumba kuelekea uwanja wa nje ukiwa na urefu wa mita 25.
8 Wakati vyumba kwenye ua wa nje vikiwa na urefu wa mita 20, vile vya mkabala na hekalu vilikuwa na urefu wa mita 50.
9 Chini ya vyumba hivi kulikuwa na njia ya kupitia tokea upande wa mashariki mwishoni mwa jengo, ikiwa mtu anaingia tokea ua wa nje
10 ambako ukuta wa nje unaanzia.Kwenye upande wa kusini kulikuwa na jengo lingine sawa na lile lingine si mbali na jengo la upande wa magharibi mwishoni mwa hekalu.
11 Mbele ya vyumba hivyo kulikuwa na njia ya kupitia kama ile ya upande wa kaskazini. Jengo hilo lilikuwa na vipimo vilevile kama vya lile lingine, ramani na miinuko yake ilifanana na ile nyingine.
12 Kulikuwa na mlango chini ya vyumba kwenye upande wa kusini wa jengo, mwishoni mwa upande wa mashariki ambako ukuta ulianzia.