30 Mtatoa pia sadaka ya nafaka na sadaka za kinywaji pamoja na hao fahali, kondoo dume na wanakondoo kulingana na idadi yao, kama inavyotakiwa.
31 Mtatoa pia beberu mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi, pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka zake za kinywaji.
32 “Siku ya saba mtatoa fahali saba, kondoo madume watatu, wanakondoo madume kumi na wanne wa mwaka mmoja, wasio na dosari.
33 Mtatoa pia sadaka ya nafaka na sadaka za kinywaji pamoja na hao fahali, kondoo dume, na wanakondoo, kulingana na idadi yao, kama wanavyotakiwa.
34 Mtatoa pia beberu mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi, licha ya ile sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka yake ya kinywaji.
35 “Siku ya nane mtakuwa na mkutano mkubwa. Msifanye kazi siku hiyo.
36 Mtatoa sadaka ya kuteketezwa iliyo harufu nzuri inayompendeza Mwenyezi-Mungu: Fahali mmoja, kondoo dume mmoja, na wanakondoo madume saba wa mwaka mmoja wasio na dosari.