40 ilikuwa watu 2,630.
41 Hii ndiyo iliyokuwa idadi ya watu wa familia za wana wa Gershoni wote waliohudumu katika hema la mkutano, ambao Mose na Aroni waliwahesabu kama Mwenyezi-Mungu alivyowaagiza.
42 Idadi ya watu wa ukoo wa Merari kufuatana na jamaa zao na familia zao,
43 wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini, waliofaa kuhudumu katika hema la mkutano,
44 ilikuwa watu 3,200.
45 Hii ndiyo idadi ya watu wa ukoo wa Merari ambao Mose na Aroni waliwahesabu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwagiza Mose.
46 Hivyo, Walawi wote walioandikishwa na Mose, Aroni na viongozi wa watu, kwa kufuata jamaa zao na koo zao,