12 Pandeni wema kwa faida yenu,nanyi mtavuna upendo;limeni mashamba yaliyoachwa,maana wakati wa kunitafuta mimi Bwana umefikanami nitawanyeshea baraka.
13 Lakini nyinyi mmepanda uovu,nyinyi mmevuna dhuluma;mmekula matunda ya uongo wenu.Wewe Israeli ulitegemea nguvu zako mwenyewe,na wingi wa askari wako.
14 Kwa hiyo msukosuko wa vita utawajia watu wako;ngome zako zote zitaharibiwa,kama Shalmani alivyoharibu Beth-arbeli vitani,kina mama wakapondwa pamoja na watoto wao.
15 Ndivyo itakavyokuwa kwenu enyi watu wa Betheli,kwa sababu ya uovu wenu mkuu.Kutakapopambazuka mfalme wa Israeli atawatokomeza.