4 Mwenyezi-Mungu asema:“Lakini mimi, Mwenyezi-Mungu, ni Mungu wenu,ambaye niliwatoa nchini Misri;hamna mungu mwingine ila mimi,wala hakuna awezaye kuwaokoeni.
5 Ni mimi niliyewatunza mlipokuwa jangwani,katika nchi iliyokuwa ya ukame.
6 Lakini mlipokwisha kula na kushiba,mlianza kuwa na kiburi, mpaka mkanisahau.
7 Basi, nitakuwa kama simba kwenu nyote;nitawavizieni kama chui njiani.
8 Nitawarukieni kama dubualiyenyang'anywa watoto wake.Nitawararua vifua vyenuna kuwala papo hapo kama simba;nitawararua vipandevipande kama mnyama wa porini.
9 “Nitawaangamiza, enyi Waisraeli.Nani ataweza kuwasaidia?
10 Yuko wapi sasa mfalme wenu awaokoe?Wako wapi wale wakuu wenu wawalinde?Nyinyi ndio mlioomba:‘Tupatie mfalme na wakuu watutawale.’