1 Enyi Waisraeli,mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.Mmejikwaa kwa sababu ya uovu wenu.
2 Ombeni toba kwake,mrudieni na kumwambia:“Utusamehe uovu wote,upokee zawadi zetu,nasi tutakusifu kwa moyo.
3 Ashuru haitatuokoa,hatutategemea tena farasi wa vita.Hatutaviita tena: ‘Mungu wetu’hivyo vinyago tulivyochonga wenyewe.Kwako ee Mungu yatima hupata huruma.”
4 Mwenyezi-Mungu asema,“Nitaponya utovu wao wa uaminifu;nitawapenda tena kwa hiari yangu,maana sitawakasirikia tena.