5 Nitakuwa kama umande kwa Waisraelinao watachanua kama yungiyungi,watakuwa na mizizi kama mwerezi wa Lebanoni.
6 Chipukizi zao zitatanda na kuenea,uzuri wao utakuwa kama mizeituni,harufu yao nzuri kama maua ya Lebanoni.
7 Watarudi na kuishi chini ya ulinzi wangu,watastawi kama bustani nzuri.Watachanua kama mzabibu,harufu yao nzuri kama ya divai ya Lebanoni.
8 Enyi watu wa Efraimu,mna haja gani tena na sanamu?Mimi ndiye ninayesikiliza sala zenu,mimi ndiye ninayewatunzeni.Mimi nitawapa kivuli kama mberoshi,kutoka kwangu mtapata matunda yenu.
9 Yeyote aliye na hekima ayaelewe mambo haya,mtu aliye na busara ayatambue.Maana njia za Mwenyezi-Mungu ni nyofu;watu wanyofu huzifuata,lakini wakosefu hujikwaa humo.”