4 Na watoto wake sitawahurumia,maana ni watoto wa uzinzi.
5 Mama yao amefanya uzinzi,aliyewachukua mimba amefanya mambo ya aibu.Alisema; “Nitaambatana na wapenzi wangu,ambao hunipa chakula na maji,sufu na kitani, mafuta na divai.”
6 Basi, nitaiziba njia yake kwa miiba,nitamzungushia ukuta,asipate njia ya kutokea nje.
7 Atawafuata wapenzi wake,lakini hatawapata;naam, atawatafuta,lakini hatawaona.Hapo ndipo atakaposema,“Nitarudi kwa mume wangu wa kwanza;maana hapo kwanza nilikuwa nafuu kuliko sasa.”
8 Hakujua kwamba ni miminiliyempa nafaka, divai na mafuta,niliyemjalia fedha na dhahabu kwa wingi,ambazo alimpelekea Baali.
9 Kwa hiyo wakati wa mavuno nitaichukua nafaka yangu,nitaiondoa divai yangu wakati wake.Nitamnyang'anya nguo zangu za sufu na kitani,ambazo zilitumika kuufunika uchi wake.
10 Nitamvua abaki uchi mbele ya wapenzi wake,wala hakuna mtu atakayeweza kunizuia.