8 Wanajishibisha kwa sadaka za watu wangu wenye dhambi.Wana hamu sana ya kuwaona wametenda dhambi.
9 Lakini yatakayowapata watu yatawapata makuhani;nitawaadhibu kwa sababu ya mwenendo wao,nitawalipiza matendo yao wenyewe.
10 Watakula, lakini hawatashiba;watazini, lakini hawatapata watoto,kwa sababu wameniacha mimi Mwenyezi-Mungu,na kufuata miungu mingine.
11 “Divai mpya na ya zamanihuondoa maarifa.
12 Watu wangu huomba shauri kutoka kwa mti;kijiti chao cha ramli ndicho kinachowapa kauli.Nia ya kufanya uzinzi imewapotosha;wamefanya uzinzi kwa kufuata miungu mingine,wakaniacha mimi Mungu wao.
13 Wanatambikia kwenye vilele vya milima;naam, wanatoa tambiko vilimani,chini ya mialoni, migude na mikwaju,maana kivuli chao ni kizuri.“Kwa hiyo binti zenu hufanya uzinzi,na bibiarusi wenu hufanya uasherati.
14 Lakini sitawaadhibu binti zenu wanapofanya uzinzi,wala bibi arusi wenu wanapofanya uasherati,maana, wanaume wenyewe ndio wanaofuatana na wazinzi,na kutambikia pamoja nao katika ibada za uzinzi.Watu hawa watovu wa akili hakika wataangamia!