10 Kiburi cha Waisraeli chashuhudia dhidi yao,hawanirudii mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao;wala hawanitafuti kwa matukio hayo yote.
11 Efraimu ni kama njiwa, mjinga asiye na akili;mara yuko Misri, mara Ashuru kuomba.
12 Watakapokwenda nitatandaza wavu wangu niwanase,nitawaangusha chini kama ndege wa angani;nitamwaadhibu kadiri ya ripoti ya maovu yao.
13 Ole wao kwa kuwa wameniacha!Maangamizi na yawapate, maana wameniasi.Nilitaka kuwakomboa,lakini wanazua uongo dhidi yangu.
14 “Wananililia, lakini si kwa moyo.Wanagaagaa na kujikatakata vitandani mwao,kusudi nisikilize dua zao za nafaka na divai;lakini wanabaki waasi dhidi yangu.
15 Mimi ndimi niliyeiimarisha mikono yao,lakini wanafikiria maovu dhidi yangu.
16 Wanaigeukia miungu batili,wako kama uta uliolegea.Viongozi wao watakufa kwa upanga,kwa sababu ya maneno yao ya kiburi.Kwa hiyo, watadharauliwa nchini Misri.