2 Miji ya Aroeri imeachwa; itakuwa kwa makundi ya kondoo, nao watajilaza huko wala hapana atakayewatia hofu.
3 Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema BWANA wa majeshi.
4 Tena itakuwa katika siku hiyo, utukufu wa Yakobo utapungua-pungua, na kunona kwa mwili wake kutakonda.
5 Tena itakuwa kama hapo avunaye ashikapo mabua ya ngano, na mkono wake ukatapo masuke; tena itakuwa kama hapo mtu aokotapo masuke katika bonde la Warefai.
6 Lakini kilichosazwa na mvunaji kitakuwa ndani yake, kama vile wakati wa kupiga mizeituni, matunda mawili matatu yaliyo juu sana; matunda manne matano katika matawi, matawi ya mti wa matunda, asema BWANA, Mungu wa Israeli.
7 Katika siku hiyo mwanadamu atamwangalia Muumba wake, na macho yake yatamtazama Mtakatifu wa Israeli.
8 Wala hataziangalia madhabahu, kazi ya mikono yake; wala hatavitazama vilivyofanyika kwa vidole vyake, maashera na sanamu za jua.