4 Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.
5 Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya BWANA.
6 Maana wewe umewaacha watu wako, nyumba ya Israeli, kwa sababu wamejaa kawaida za mashariki, nao ni wapiga ramli kama Wafilisti, na wanapana mikono na wana wa wageni.
7 Tena nchi yao imejaa fedha na dhahabu, wala hapana mwisho wa hazina zao; tena nchi yao imejaa farasi, wala hapana mwisho wa magari yao.
8 Tena nchi yao imejaa sanamu; huabudu kazi ya mikono yao, vitu vilivyofanywa kwa vidole vyao wenyewe.
9 Mtu mnyonge huinama, na mtu mkubwa hujidhili; kwa hiyo usiwasamehe.
10 Ingia ndani ya jabali; ukajifiche mavumbini mbele za utisho wa BWANA, mbele za utukufu wa enzi yake.