8 Naam, katika njia ya hukumu zakoSisi tumekungoja, Ee BWANA;Shauku ya nafsi zetu inaelekeaJina lako na ukumbusho wako.
9 Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku;Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema;Maana hukumu zako zikiwapo duniani,Watu wakaao duniani hujifunza haki.
10 Mtu mbaya ajapofadhiliwa,Hata hivyo hatajifunza haki;Katika nchi ya unyofu atatenda udhalimu,Wala hatauona utukufu wa BWANA.
11 BWANA, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.
12 BWANA, utatuamuria amani; maana ni wewe pia uliyetutendea kazi zetu zote.
13 Ee BWANA, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako.
14 Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajilia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao.