18 Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari;
19 Tena wazao wako wangalikuwa kama mchanga, na hao waliotoka katika tumbo lako kama chembe zake; jina lake lisingalikatika, wala kufutwa mbele zangu.
20 Haya, tokeni katika Babeli,Kimbieni kutoka kwa Wakaldayo;Hubirini kwa sauti ya kuimba, tangazeni haya,Yatamkeni mpaka mwisho wa dunia, semeni,BWANA amemkomboa mtumishi wake, Yakobo.
21 Wala hawakuona kiu alipowaongoza jangwani;Alitoa maji katika mwamba kwa ajili yao;Pia akaupasua mwamba, maji yakatoka kwa nguvu.
22 Hapana amani kwa wabaya, asema BWANA.