3 Yeye achinjaye ng’ombe ni kama yeye amwuaye mtu; na yeye atoaye dhabihu ya mwana-kondoo ni kama yeye avunjaye shingo ya mbwa; na yeye atoaye matoleo ni kama yeye atoaye damu ya nguruwe; na yeye afukizaye uvumba ni kama yeye abarikiye sanamu; naam, wamezichagua njia zao wenyewe, na nafsi zao zafurahia machukizo yao.
4 Mimi nami nitachagua mapigo yao, nitaleta hofu zao juu yao; kwa sababu nilipoita, hawakuitika; na niliponena, hawakusikia; bali walifanya yaliyo maovu machoni pangu, na kuyachagua nisiyoyafurahia.
5 Lisikilizeni neno la BWANA, ninyi mtetemekao kwa sababu ya neno lake; Ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina langu, wamesema, Na atukuzwe BWANA, tupate kuiona furaha yenu; lakini watatahayarika.
6 Sauti ya fujo itokayo mjini!Sauti itokayo hekaluni!Sauti ya BWANA awalipaye adui zake adhabu!
7 Kabla hajaona utungu alizaa;Kabla maumivu yake hayajampata,Alizaa mtoto mwanamume.
8 Ni nani aliyesikia neno kama hili?Ni nani aliyeona mambo kama haya?Je! Nchi yaweza kuzaliwa siku moja?Taifa laweza kuzaliwa mara?Maana Sayuni, mara alipoona utungu,Alizaa watoto wake.
9 Je! Mimi nilete wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? Asema BWANA; mimi nizalishaye, je! Nilifunge tumbo? Asema Mungu wako.