20 Hivyo ndivyo mwendo wa mwanamke mzinifu;Hula, akapangusa kinywa chake,Akasema, Sikufanya uovu.
21 Kwa ajili ya mambo matatu nchi hutetemeka,Naam, kwa ajili ya manne haiwezi kuvumilia.
22 Mtumwa apatapo kuwa mfalme;Mpumbavu ashibapo chakula;
23 Mwanamke mwenye kuchukiza aolewapo;Na mjakazi aliye mrithi wa bibi yake.
24 Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo;Lakini vina akili nyingi sana.
25 Chungu ni watu wasio na nguvu;Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari.
26 Wibari ni watu dhaifu;Lakini hujifanyia nyumba katika miamba.