1 Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:
2 “Kwa nini mnarudiarudia methali hii katika nchi ya Israeli:‘Akina baba wamekula zabibu mbichi,lakini meno ya watoto wao yakatiwa ganzi!’
3 Lakini, kama niishivyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nasema kwamba methali hii haitatumika tena katika Israeli.
4 Jueni kwamba uhai wote ule ni wangu, uhai wa mzazi na uhai wa mtoto. Yeyote anayetenda dhambi, ndiye atakayekufa.
5 “Kama mtu ni mwadilifu, anafuata yaliyo haki na sawa,
6 kama hashiriki tambiko za sanamu za miungu mlimani wala kuzitegemea sanamu za miungu ya Waisraeli, kama hatembei na mke wa jirani yake wala kulala na mwanamke wakati wa siku zake,