2 Jengo hili lililokuwa upande wa kaskazini lilikuwa na urefu wa mita 50 na upana wa mita 25.
3 Kulikuwako ghorofa tatu zilizounganisha mita 10 za ua wa ndani na zikiwa mkabala wa sakafu ya ua wa nje.
4 Upande wa kaskazini wa jengo hilo, kulikuwa na njia ya kupitia yenye upana wa mita 5 na urefu wake mita 50. Milango yake ilikuwa upande wa kaskazini.
5 Vyumba vya juu vilikuwa vyembamba kuliko vile vya katikati na vya chini kwani vilikuwa mbali zaidi.
6 Vile vyumba vya juu kabisa vilijengwa kwenye miinuko na havikusaidiwa na nguzo kama majengo mengine kwenye ua wa nje.
7 Kulikuwa na ukuta mkabala na vyumba kuelekea uwanja wa nje ukiwa na urefu wa mita 25.
8 Wakati vyumba kwenye ua wa nje vikiwa na urefu wa mita 20, vile vya mkabala na hekalu vilikuwa na urefu wa mita 50.