10 Kila mtu ni lazima atumie mizani na vipimo halali.
11 Kwa kipimo cha ulinganifu: Efa kwa nafaka na bathi kwa mafuta zina kiasi sawa. Hivyo viwili ni moja ya kumi ya homeri moja.
12 Kwa kupimia uzani: Gera 20 ni shekeli moja, shekeli 50 ni mina moja.
13 “Vipimo vya matoleo yenu ya nafaka vitakuwa hivi: Moja ya sita ya efa katika homeri moja ya ngano, na moja ya sita ya efa katika homeri moja ya shayiri.
14 Kiwango cha mafuta kitakuwa hivi: Moja ya bathi ya mafuta kutoka kila kori (kori moja ni sawa na homeri moja ambayo ni sawa na bathi kumi).
15 Watatoa kondoo mmoja kwa kila kundi la kondoo 200 katika jamaa za Israeli. Wataleta sadaka za nafaka, sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, ili wapate kufanyiwa upatanisho. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.
16 Watu wote nchini watampa sadaka hizo mtawala wa Israeli.