12 Balaamu akamjibu Balaki, “Je, sikuwaambia wajumbe uliowatuma kwangu
13 kwamba hata kama ungenipa nyumba yako imejaa fedha na dhahabu, mimi sitaweza kukiuka agizo la Mwenyezi-Mungu, kwa kufanya jambo lolote, jema au baya kwa hiari yangu mwenyewe? Nilisema, atakachosema Mwenyezi-Mungu ndicho nitakachokisema.
14 “Sasa ninarudi kwa watu wangu, lakini kabla sijaondoka, acha nikuambie mambo ambayo watu hao watawatendea watu wako siku zijazo.”
15 Basi, Balaamu akatamka kauli hii:“Kauli yangu mimi Balaamu mwana wa Beori,kauli ya mtu aliyefumbuliwa macho,
16 kauli ya mtu aliyesikia maneno ya Mungu,na mtu ajuaye maarifa ya Mungu Mkuu,mtu aonaye maono ya Mungu Mwenye Nguvu,mtu anayesujudu, macho wazi.
17 Ninamwona, atakayekuja, lakini baadaye,namwona, lakini hayuko karibu.Nyota itatokea kwa wazawa wa Yakobo,atatokea mfalme miongoni mwa Waisraeli.Kwa fimbo yake atawachapa viongozi wa Wamoabuatawaangamiza wazawa wote wa Sethi.
18 Edomu itamilikiwa naye,Seiri itakuwa mali yake,Israeli itapata ushindi mkubwa.