4 Wanachosema ni maneno matupu;wanaapa na kufanya mikataba ya bure;haki imekuwa si haki tena,inachipua kama magugu ya sumu shambani.
5 Wakazi wa Samaria watatetemekakwa sababu ya ndama wa huko Betheli.Watu wake watamwombolezea ndama huyo,hata makuhani wanaomwabudu watamlilia;kwani fahari ya ndama huyo imeondolewa.
6 Kinyago hicho kitapelekwa Ashuru,kama ushuru kwa mfalme mkuu.Watu wa Efraimu wataaibishwa,Waisraeli watakionea aibu kinyago chao.
7 Mfalme wa Samaria atachukuliwa,kama kipande cha mti juu ya maji.
8 Mahali pa kuabudia vilimani pa Aweni,dhambi ya Waisraeli, pataharibiwa.Miiba na magugu vitamea katika madhabahu zao.Nao wataiambia milima, “Tufunikeni”na vilima, “Tuangukieni!”
9 Enyi Waisraeli,nyinyi mmetenda dhambi tangu kule Gibea,na bado mnaendelea.Hakika vita vitawaangamiza hukohuko Gibea.
10 Nitawajia watu hawa wapotovu na kuwaadhibu;watu wa mataifa watakusanyika kuwashambulia,watakapoadhibiwa kwa ajili ya dhambi zao nyingi.