3 Mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea!Mimi mwenyewe niliwachukua mikononi mwangu;lakini hawakutambua kuwa mimi ndiye niliyewatunza.
4 Niliwaongoza kwa kamba za hurumanaam, kwa kamba za upendo;kama baba amwinuaye mtoto mpaka shavuni mwake,ndivyo nami nilivyokuwa kwao.Mimi niliinama chini na kuwalisha.
5 Basi, watarudi nchini Misri;watatawaliwa na mfalme wa Ashuru,kwa sababu wamekataa kunirudia.
6 “Upanga utavuma katika miji yao,utavunjavunja miimo ya malango yakena kuwaangamiza katika ngome zao.
7 Watu wangu wamepania kuniacha mimi,wakiitwa waje juu,hakuna hata mmoja anayeweza.
8 Ewe Efraimu, nawezaje kukuacha?Nawezaje kukutupa ewe Israeli?Nitawezaje kukufanya kama mji wa Adma?Nitawezaje kukutenda kama Seboimu!Nazuiwa na moyo wangu;huruma yangu imezidi kuwa motomoto.
9 Nitaizuia hasira yangu kali;sitamwangamiza tena Efraimu,maana mimi ni Mungu, wala si binadamu.“Mimi ndimi Mtakatifu miongoni mwenu,nami sitakuja kuwaangamiza.