2 Ombeni toba kwake,mrudieni na kumwambia:“Utusamehe uovu wote,upokee zawadi zetu,nasi tutakusifu kwa moyo.
3 Ashuru haitatuokoa,hatutategemea tena farasi wa vita.Hatutaviita tena: ‘Mungu wetu’hivyo vinyago tulivyochonga wenyewe.Kwako ee Mungu yatima hupata huruma.”
4 Mwenyezi-Mungu asema,“Nitaponya utovu wao wa uaminifu;nitawapenda tena kwa hiari yangu,maana sitawakasirikia tena.
5 Nitakuwa kama umande kwa Waisraelinao watachanua kama yungiyungi,watakuwa na mizizi kama mwerezi wa Lebanoni.
6 Chipukizi zao zitatanda na kuenea,uzuri wao utakuwa kama mizeituni,harufu yao nzuri kama maua ya Lebanoni.
7 Watarudi na kuishi chini ya ulinzi wangu,watastawi kama bustani nzuri.Watachanua kama mzabibu,harufu yao nzuri kama ya divai ya Lebanoni.
8 Enyi watu wa Efraimu,mna haja gani tena na sanamu?Mimi ndiye ninayesikiliza sala zenu,mimi ndiye ninayewatunzeni.Mimi nitawapa kivuli kama mberoshi,kutoka kwangu mtapata matunda yenu.