1 Neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Yeremia kuhusu ule ukame:
2 “Watu wa Yuda wanaomboleza,na malango yao yanalegea.Watu wake wanaomboleza udongonina kilio cha Yerusalemu kinapanda juu.
3 Wakuu wake wanawatuma watumishi wao maji;watumishi wanakwenda visimani,lakini maji hawapati;wanarudi na vyombo vitupu.Kwa aibu na fadhaa wanafunika vichwa vyao.
4 Wakulima wanahuzunika na kufunika vichwa vyaokwa kuona jinsi ardhi ilivyonyauka.
5 Hata kulungu porini anamwacha mtoto wake mchanga,kwa sababu hakuna nyasi.
6 Pundamwitu wanasimama juu ya vilele vikavu,wanatweta kwa kukosa hewa kama mbweha;macho yao yanafifia kwa kukosa chakula.
7 “Nao watu wanasema:Ingawa dhambi zetu zashuhudia dhidi yetu,utusaidie ee Mwenyezi-Mungu kwa heshima ya jina lako.Maasi yetu ni mengi,tumetenda dhambi dhidi yako.