Yeremia 49 BHN

Waamoni

1 Kuhusu Waamoni.Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Je, Israeli hana watoto?Je, hana warithi?Mbona basi mungu Milkomu amemiliki Gadina watu wake kufanya makao yao mijini mwake?

2 Basi, wakati unakuja kweli, siku zaja,nasema mimi Mwenyezi-Mungu,ambapo nitavumisha sauti ya vitadhidi ya Raba mji wa Waamoni.Raba utakuwa rundo la uharibifu,vijiji vyake vitateketezwa moto;ndipo Israeli atakapowamiliki wale waliomiliki.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

3 “Ombolezeni, enyi watu wa Heshboni,maana mji wa Ai umeharibiwa!Lieni enyi binti za Raba!Jifungeni mavazi ya gunia viunoniombolezeni na kukimbia huko na huko uani!Maana mungu Milkomu atapelekwa uhamishoni,pamoja na makuhani wake na watumishi wake.

4 Mbona mnajivunia mabonde yenu, enyi msioamini,watu mliotegemea mali zenu, mkisema:‘Nani atathubutu kupigana nasi?’

5 Basi, mimi nitawaleteeni vitishokutoka kwa jirani zenu wote,nanyi mtafukuzwa nje kila mtu kivyake,bila mtu wa kuwakusanya wakimbizi.Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.

6 Lakini baadaye nitawarudishia Waamoni fanaka yao.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Edomu

7 Kuhusu Edomu.Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi:“Je, hakuna tena hekima mjini Temani?Je, wenye busara wao hawana shauri tena?Hekima imetoweka kabisa?

8 Kimbieni enyi wakazi wa Dedani;geukeni mkaishi mafichoni!Maana nitawaleteeni maangamizienyi wazawa wa Esau;wakati wa kuwaadhibu umefika.

9 Wachuma zabibu watakapokuja kwenuhawatabakiza hata zabibu moja.Usiku ule wezi watakapofika,wataharibu kila kitu mpaka watosheke.

10 Lakini nimemnyanganya Esau kila kitu,naam, nimeyafunua maficho yake,wala hawezi kujificha tena.Watoto, ndugu na jirani zake wameangamizwa;hakuna hata mmoja aliyebaki.

11 Niachieni watoto wenu yatima nami nitawatunza;waacheni wajane wenu wanitegemee.”

12 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Ikiwa wale ambao hawakustahili kunywa kikombe cha adhabu ni lazima wanywe, je, wewe utaachwa bila kuadhibiwa? La! Hutakosa kuadhibiwa; ni lazima unywe hicho kikombe!

13 Maana nimeapa kwa nafsi yangu kwamba mji wa Bosra utakuwa kioja na kichekesho, utakuwa uharibifu na laana; vijiji vyote vitakuwa magofu daima. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

14 Nimepata habari kutoka kwa Mwenyezi-Mungu,mjumbe ametumwa ayatangazie mataifa:“Jikusanyeni pamoja dhidi ya Edomu;inukeni mwende kuushambulia!

15 Mimi Mwenyezi-Mungu nitakufanya wee Edomukuwa mdogo kuliko mataifa yote.Ulimwengu wote utakudharau.

16 Vitisho unavyotoa na kiburi chako vimekudanganya,ewe ukaaye katika mapango ya miamba,unayeishi juu ya kilele cha mlima!Ingawa unaweka makao yako juu kama ya tai,mimi nitakuporomosha kutoka huko uliko.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

17 “Edomu itakuwa kitisho na kila mtu atakayepita karibu yake atashangaa, na kuizomea kwa sababu ya maafa yatakayoipata.

18 Kama vile Sodoma na Gomora na miji jirani yake ilivyoangamizwa, mimi Mwenyezi-Mungu nasema, hakutakuwa na mtu yeyote atakayeishi Edomu wala kufanya mashauri humo.

19 Kama vile simba anavyochomoza kutoka msitu wa mto Yordani na kuingia kwenye malisho mazuri, ndivyo nitakavyowafukuza ghafla Waedomu kutoka nchi yao. Nami nitamweka huko kiongozi yeyote nitakayemchagua. Maana, ni nani anayeweza kulinganishwa nami? Nani awezaye kunishtaki? Ni mchungaji gani awezaye kunipinga?

20 Kwa hiyo, sikilizeni mpango ambao mimi Mwenyezi-Mungu nimepanga dhidi ya Edomu pamoja na mambo niliyokusudia kuwafanyia wakazi wa Temani: Hakika, watoto wao wadogo wataburutwa na kuchukuliwa; kweli kutakuwa na mshangao mkubwa katika makao yao!

21 Kwa kishindo cha kuanguka kwao, dunia itatetemeka; sauti ya kilio chao itasikika mpaka bahari ya Shamu.

22 Tazama, adui atapanda juu na kuruka kama tai na kutandaza mabawa yake juu ya Bosra. Siku hiyo moyo wa mashujaa wa Edomu utakumbwa na hofu kama ya mwanamke anayejifungua.”

Damasko

23 Kuhusu Damasko:“Miji ya Hamathi na Arpadi, imejaa wasiwasikwa kufikiwa na habari mbaya;mioyo ya watu wake inayeyuka kwa hofu,imefadhaika kama bahari isiyoweza kutulia.

24 Watu wa Damasko wamekufa moyo;wamegeuka wapate kukimbia;hofu kubwa imewakumba,uchungu na huzuni vimewapata,kama mwanamke anayejifungua

25 Ajabu kuachwa kwa mji maarufu,mji uliokuwa umejaa furaha!

26 Basi vijana wake wataanguka viwanjani mwake,askari wake wote wataangamizwa siku hiyo.Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.

27 Nitawasha moto katika kuta za Damasko,nao utateketeza ngome za mfalme Ben-hadadi.”

Makabila ya Kedari na Hazori

28 Kuhusu Kedari na falme za Hazori ambazo Nebukadneza mfalme wa Babuloni, alizishambulia na kuzishinda, Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Inuka uende kulishambulia kabila la Kedari!Waangamize watu wa mashariki!

29 Hema zao na kondoo wao vitachukuliwa,kadhalika mapazia yao na mali yao yote;watanyanganywa ngamia wao,na kilio kitasikika: ‘Kitisho kila upande!’

30 Kimbieni, nendeni mbali, kaeni mashimoni.Enyi wakazi wa Haziri,kimbieni mtangetange na kukaa mafichoni!Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.Maana Nebukadneza mfalme wa Babuloni,amefanya mpango dhidi yenu,amepania kuja kuwashambulia.

31 Inuka uende kulishambulia taifa linalostarehe,taifa linaloishi kwa usalama.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.Taifa hilo halina malango wala pao za chuma;ni taifa ambalo liko peke yake.

32 “Ngamia wao watatekwamifugo yao itachukuliwa mateka.Nitawatawanya kila upande,watu wale wanaonyoa denge.Nitawaletea maafa kutoka kila upande.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

33 Mji wa Hazori utakuwa makao ya mbweha,utakuwa jangwa daima;hakuna mtu atakayekaa humo,wala atakayeishi humo.”

Elamu

34 Neno la Mwenyezi-Mungu lililomjia nabii Yeremia kuhusu Elamu, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia, mfalme wa Yuda.

35 Mwenyezi-Mungu wa majeshi, asema hivi: “Nitavunja upinde wa watu wa Elamu ulio msingi wa nguvu zao.

36 Nitaleta upepo kutoka pande zote za mbingu; nitawatawanya kila mahali, wala hapatakuwa na taifa lolote ambalo halitakuwa na wakimbizi wa Elamu.

37 Nitawafadhaisha watu wa Elamu mbele ya maadui zao na mbele ya wale wanaotaka kuyaangamiza maisha yao. Nitawaletea maafa na hasira yangu kali. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Nitawaletea upanga kuwafuata mpaka niwaangamize kabisa.

38 Nitaweka kiti changu cha enzi huko Elamu na kumwangamiza mfalme wao pamoja na wakuu wao. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

39 Lakini katika siku za mwisho, nitaurudishia mji wa Elamu fanaka yake. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”